Botanix – Jarida kuhusu mimea

Toleo la Kiswahili

Khasi Pine (Pinus kesiya)

Khasi Pine (Pinus kesiya) ni spishi inayokua haraka sana kutoka Asia, ambayo mara nyingi haipatikani kwenye maeneo mengine nje ya nchi yake. Miti hii ina urefu wa takribani mita 30–35 na magogo yake yanaweza kufika hadi upana wa m 1. Kila tawi lina spines tatu – kila mmoja una urefu wa karibu sm 15 hadi 20. Matunda ya miti hii ina urefu wa karibu sm 5 hadi 9 na mbegu zake karibu sm 1,5 hadi 2,5.

Asili ya Khasi Pine (Pinus kesiya) ni mkoa wa Himalaya: kutoka Kaskazini – Mashariki mwa India (siku hizi kutokana na kiwanda cha mbao tu katika mlima wa Khasi na mlima Naga kwenye eneo la Meghalay na Manipur), China (the Yunnan province), Burma (Myanmar), Kusini mwa Tailandi, Laos, Vietinam (Lai Chau, Lang Son, Cao Bang, Quang Ninh) na Ufilipino (Luzon). Pines kutoka Ufilipino mara kadhaa hutambulika kama spishi ya pekee inayoitwa Pinus insularis. Huko China mtu mmoja aliona spishi inayofanana na hiyo inayoitwa Yunnan Pine (Pinus yunnanensis)

Hizi spishi zinapatikana kwenye maeneo ya mteremko na mchanganyiko wa miti inayokua kwenye udongo wenye kiwango kidogo cha viunguza vyekundu na vya njano (pH of 4,5), na kimo cha mita 800–2000 lakini mara nyingi ni kati ya m 1200–1400. Eneo ni la joto kiasi pamoja na mabadiliko wakati wa kipindi cha unyevunyevu na ukame katika mwaka. Mvua ni kubwa na hali ya hewa kwenye eneo ni joto kiasi na kuna mabadiliko ya vipindi vya unyevunye na ukame katika mwaka, na mvua kubwa na unyevu wa zaidi ya 70%.

Mmea huu huhimili kidogo baridi, lakini huathirika haraka baridi inapochelewa wakati wa uoteshaji. Hata hivyo, wakati wa kilimo inahitaji eneo ambalo halina baridi kali.

Majina mengine ya mmea: Pinus khasya, Pinus khasyanus

««« Makala iliyopita: Mti wa mfune wa India Pongamia pinnata Makala inayofuata: Michikichi Parajubaea torallyi »»»

Jumapili 9.8.2009 11:23 | chapa | Konifa

Kuhusu KPR

KPR - Klabu ya Wakulima wa Bustani Slovakia
KPR - Klabu ya Wakulima wa Bustani ni shirika la kimataifa la wakulima wa bustani. Soma zaidi...
Shirikisha uzoefu wako kuhusu ukuzaji mimea. Andika makala kuhusu ukulima wa bustani, mimea, upandaji wa mimea nk. na uichapishe kwenye toleo la lugha yako la jarida letu la Botanix! Wasiliana nasi kwa taarifa zaidi.