Botanix – Jarida kuhusu mimea

Toleo la Kiswahili

Upandaji wa nyasi kwenye uwanja mpya

Ulaya wakati mzuri wa kupanda mpya kwenye uwanja mpya au majani zaidi kwenye uwanja uliopo ni kuanzia Mei hadi Juni. Iwapo kuna mvua ndogo wakati wa uoto, Julai unaweza kuwa wakati mzuri kupanda.

Upandaji wa nyasi kwenye uwanja mpya

Eneo ambalo ungependa kupanda nyasi mpya lazima uchimbe urefu wa sentimita 10–15. Unaweza sasa kusawazisha udongo kwa kutumia mashine ya sandazia udongo.

Sasa una vitu viwili vinavyowezena:

a) Ufukiaji wa mbegu za majani

Kwanza, unatakiwa kupima usawa wa eneo ambalo unataka kupanda. Kisha piga hesabu kiasi gani cha mbegu utahitaji. Kumbuka kwamba utahitaji gramu 25 za mbegu kwa kila mita 1. Kwa kuongezea, utahitaji gramu 25 zaidi kwa kila mita 10. Zaidi ya hayo, ona kwamba mbegu zako ni mpya unapozinunua kwani mbegu za majani hupoteza nguvu zake za kuota kwa haraka. (Nguvu za kuota za mbegu zenye umri wa miaka miwili ni chini zaidi ya asilimia 50). Tafadhali zingatia pia mbegu imehifadhiwa kwa namna gani dukani (kama mbegu ina unyevunyevu, au baadhi ya mbegu tayari zimeota, ni vyema usinunue mbegu hizo – hivyo unaweza kuzuia matatizo yasiyo ya lazima). Bei ya mbegu za majani hubadilika kutoka Euro 3/ kilogramu (kutegemea na aina).

Chagua mbegu zako kwa kuzingatia matumizi ya uwanja wako wa nyasi (utatembea juu yake tu, kukumbia, kufanyia mazoezi au utautumia kwa ajili ya wanyama). Wauzaji makini watakuwa na vipeperushi vyenye taarifa za kukusaidia na chaguo lako la mbegu miongoni mwa chaguzi nyingi za mbegu. Maduka ya uhakika yatatoa hivi vipeperushi kwa wateja wake kwa maombi. Kamwe usinunue mbegu bila taarifa kusudiwa.

Weka mbegu kwenye sehemu yenye baridi na kavu baada ya kuinunua. Tunashauri sana kwamba usiweke mbegu kwa zaidi ya mwaka mmoja kwani inapoteza kw aharaka nguvu zake za kuota. Ipande Mei au Juni. Kabla ya kupanda, tumia reki na tengeneza mfuo wa sentimita 1 kwenye ardhi. Baada ya kupanda, tandaza eneo (kwa kutumia mashine ya kutandazia kwa mfano) na inyunyizie vizuri. Mbegu itaanza kuchipua ndani ya siku 14. Majani yakifikia urefu wa sentimita 10, lazima yafyekwe kwa mara ya kwanza. Kama utaona mabaka yasiyo na nyasi kwenye uwanja wako sasa, unaweza kupanda mbegu zingine zaidi kwenye maeneo haya. Iwapo ungependa zulia la majani membamba na mazuri, ungetakiwa kufyeka mara moja hadi mbili kwa kila wiki mbili hadi Septemba.

b) Tumia vigae vya majani kwa uwanja wako Hii ni haraka, lakini ni njia ya gharama. Kwa namna yoyote ina faida zaidi kwasababu makampuni mengi yanauza vigae vya majani, pamoja na kuviweka chini, katika bei. Bei za vigae vya majani, pamoja na kazi, hubadilika kutoka kati ya Euro 5/m2 (inategemea na aina)

2. Matengenezo ya uwanja wa nyasi wa zamani Chakura uwanja wote kutoa majani na nyasi zilizokauka kila marija ya kuchipua (kutegemea na hali ya hewa katika Ulaya wakati wa Machi hadi Mei. Kasha panda mbegu zaidi kama ni lazima. Uwanja unaweza “kuchukuliwa” na barafu wakati wa baridi kali na hivyo bora kuutandaza wakati wa majira ya kuchipua.

Matengenezo ya uwanja wako yanahamasishwa na hewa nzuri kwenye ardhi. Kwa hii, unaweza kutengeneza nyenzo rahisi mwenyewe. Chukua ubao mwembamba wenye sentimita 2–3, Misumari ya urefu wa sentimita 10 igongomee kwenye ubao ili itokeze upande mwingine. Hakikisha kwamba misumari inaachana kwa sentimita 2–3. Weka mshikio wa mbao kwenye mmea (urefu ulingane na wewe ili kukuwezesha kuushika vizuri)

Sasa chukua ubao na uweke uwanjani (baada ya kufyeka) na simama imara juu ya ubao. Sasa vuta nje na rudia kumaliza uwanja wako wote. Unaweza pia kutumia reki. Iwapo unataka kumwagilia uwanja wako, unaweza kufanya hivi baada ya kuupa hewa uwanja. Maji sasa yatafikia mizizi kwa urahisi.

««« Makala iliyopita: Ulimaji wa Klova ya majani manne - (Marsilea quadrifolia) Makala inayofuata: Jinsi gani ya kufyeka nyasi za uwanja wako kwa usahihi? »»»

Ijumaa 22.7.2011 08:52 | chapa | Majani

Kuhusu KPR

KPR - Klabu ya Wakulima wa Bustani Slovakia
KPR - Klabu ya Wakulima wa Bustani ni shirika la kimataifa la wakulima wa bustani. Soma zaidi...
Shirikisha uzoefu wako kuhusu ukuzaji mimea. Andika makala kuhusu ukulima wa bustani, mimea, upandaji wa mimea nk. na uichapishe kwenye toleo la lugha yako la jarida letu la Botanix! Wasiliana nasi kwa taarifa zaidi.