Botanix – Jarida kuhusu mimea

Toleo la Kiswahili

Jinsi gani ya kushambulia wadudu walao nafaka?

Nadhanii kwamba wadudu walao nafaka wanahitaji hawatakiwi kutambulishwa kwako. Huyu ni mende mdogo wa ukubwa wa mm 3–4, ambaye anaweza kupatikana kwenye mbegu jikoni kwa mfano.

Hawa wadudu wadogo waharibifu hukua kwenye mbegu za aina zote za maganda. Ukweli, kila ganda lina viumbe hawa – wadudu walaomaharage (mende), mende wa njegere, mende wa dengu, na mende wa kwenye bustani n.k…

Kwenye mbegu zilizoharibika unaweza kuona michubuko kwenye maeneo ambapo matundu madogo wamechimbwa na viwavi. Mende wakubwa wanapozaliwa, mashimo yaliyochimbwa yanakuwa hayaonekani kwenye mbegu. Mende mara kwa mara husababisha uharibifu mkubwa wakati wa kipindi cha kuhifadhi (kwasababu hali ya maisha ni nzuri) bilakujali ukweli kwamba mmea tayari ulishaathiriwa wakati bado ukiwa bustanini.

Mapambano dhidi ya mende ni rahisi kabisa na mathubuti (nafasi ya kushinda kwa ailimia 100!)

foto

Mende wakiwa kwenye mbegu za Erythrina lysistemon

Mara tu baada ya kuchagua maganda na mbegu zilizoiva, zimenye na ziache zikauke, na hakikisha kwamba hakuna mbegu zilizoathiriwa kati yake. Tupa mbegu zote zilizoharibika (njia sahihi ni kuzichoma). Baada ya hapo weka mbegu kwenye mfuko wa plastiki au pamba na ziweke kwenye sehemu ya kugandishia kwenye friji kwa saa 48. Kwa njia hii unaweza kuharibu hatua ya ukuaji ya mende.

Baada ya kuzitoa mbegu kwenye sehemu ya kugandishia kwenye friji, unaweza sasa kuzikausha kwa kati ya siku 2–3 kwenye joto la kawaida. Unaweza kuziacha mbegu kwenye mfuko wa plastiki hadi utakapotaka kuzitumia. Mbegu zilizohifadhiwa kwa njia hii zinaweza kuathiriwa tu na mbegu zilizonunuliwa dukani.

Kwa sababu hii, ni bora kuhifadhi mbegu zako kwenye chupa ya kioo na kifuniko. Mbegu lazima ikauke kabisa vinginevyo, itaoza. Njia hii unaweza kunaweza kuhakikisha kwamba mbegu zako hazitaathiriwa na mende.

Wadudu walao nafaka wanaweza pia kuthibitiwa kwa kuchaua mbegu sahihi – kuna aina nyingi ambayo wadudu walao nafaka hawapendi.

««« Makala iliyopita: Ukuzaji wa Uyoga chaza (Pleurotus ostreatus) Makala inayofuata: NOVODOR FC kwa kupambana na mdudu aina ya Colorado anayeharibu nyanya »»»

Jumanne 12.7.2011 17:07 | chapa | Wadudu

Kuhusu KPR

KPR - Klabu ya Wakulima wa Bustani Slovakia
KPR - Klabu ya Wakulima wa Bustani ni shirika la kimataifa la wakulima wa bustani. Soma zaidi...
Shirikisha uzoefu wako kuhusu ukuzaji mimea. Andika makala kuhusu ukulima wa bustani, mimea, upandaji wa mimea nk. na uichapishe kwenye toleo la lugha yako la jarida letu la Botanix! Wasiliana nasi kwa taarifa zaidi.