Botanix – Jarida kuhusu mimea

Toleo la Kiswahili

Mti wa Tumbaku Nicotiana glauca – mmea wa roshani wenye tumaini!

foto

Tumbaku (Nicotiana glauca)

Hitaji la mwanadamu kufanya kitu kipya na kisicho cha kawaida halizuiliki. Hivyo wakulima wa bustani pia wanaota kulima kitu kipya kwenye bustani zao – kitu ambacho hakuna mtu mwingine mwenye nacho. Soko la mimea kwahiyo huwapa wakulima wa bustani kitu kipya kila siku – kuiba njaa ya wakulima wa bustani kutafuta kitu Fulani cha asili kutosheleza mahitaji yao. Uzinduzi wa kibiashara wa aina mpya utaufanya mmea wa tumbaku kujulikana kwa wakulima wote wa bustani hivi karibuni.

foto

Tumbaku (Nicotiana glauca)

Katika miongo kumi iliyopita uvumbuzi mkubwa katika ulimwengu wa mimea umekuja kutoka kwenye familia ya mtunguja (Solanaceae). Inayojulikana sana katika hii ni petunia, surfinia, na million bells (Calibrachoa). Siri ya mafanikio yake huegemea katika ukuaji wao wa haraka, utoaji wa maua mapema (inapootesha kutoka mbegu huchanua ndani ya miezi 3, na inapooteshwa kipandikizi huchanua haraka sana) na ukweli hazihitaji hali maalumu kukua. Zinapendelea maeneo yenye jua, lakini panda pia kwenye maeneo ya giza na baridi.

Hata hivyo, mimea kutoka kwenye familia ya mtunguja hazikujulikana wakati wote. Fikiria mfano wa viazi na nyanya ambayo ilipandwa kwa mara moja tu kutokana na uzuri wake! Zilipokuja habari kwamba mimea hii ingeweza kuliwa, mtu mwanzoni alikuwa na wasiwasi. Sasa inaliwa kwa wingi katika nchi nyingi na hata vyakula vya kitamaduni vimeweka nafasi kwa mimea hii!

foto

Kwenye habari hii tutatambulisha kwako mmea wa Tumbaku (Nicotiana glauca) – mmea roshani usiyo wa kawaida asili yake Amerika ya Kusini. Ni kichaka au mti unaokua kwa haraka. Huanza kuchanua baada ya miezi miwili tu baada ya kupandwa, na matawi ya mimea mikubwa inakua had ism 50–70 ndani ya mwezi mmoja.

Kama vile jina lake la Kilatini linavyosadikiwa (glauca = kijivu), mmea uliokamilika una rangi ya fedha kijivu. Hivyo, lazima usishikwe kwani hupoteza mng’aro wa rangi yake kwa urahisi na kubadili mmea kuwa katika rangi isiyovutia ya kijani mpauko. Majani ni ya fedha na kijivu, lipo kama yai na lenye ncha mwishoni. Mwisho wa matawi ni matawi madogo yenye maua ya njano yapatayo 20 –40. Maua yana urefu wa sm 3–3,5 na upana wa sm 0,5. maua yanapoanza kutoka yanakuwa na rangi ya niano mpauko na ncha zenye rangi ya kijani mpauko. Baada ya kuchanua, yanabadilika na kuwa rangi ya njano iliyokolea. Faida ya mmea huu ni kwamba maua yanafaa kwa kupamba hata baada ya kuchanua. Tofauti na mfano Petunia, maua ya mmea huu hutunza muundo wake na kuendelea kuning’inia kwenye tawi kwa uda mrefu.

Upandaji wa aina hii ni rahisi. Unaweza kuweka mti wa tumbaku (Nicotiana glauca) ndani ya nyumba au nje wakati wa majira ya joto. Unaweza ukaizidisha kwa kutumia mbegu, ambazo huota kwa haraka na zina nguvu kubwa ya kuota. Mmea utaanza kuchanua ndani ya miezi miwili (hivyo iwapo unataka uwe na maua mengi kunzia mei, utatakiwa kupanda mwezi machi).

Kama unaishi kwenye maeneo ambayo barafu hutokea, unatakiwa kuweka tumbaku sehemu isiyo na barafu. Na Pelargonium, unaweza kuweka mimea hii kwenye baridi (lakini angavu) weka kwenye baridi. Mwisho wa baridi, unaweza kupunguza matawi kwa nusu na ipe maji mengi. Mmea wa tumbaku utachanua ndani ya mwezi. Mmea huu unaweza kutengeneza kwa urahisi mti, ambao unaweza kuuweka ndani ya nyumba yako. Hatahivyo huwezi kuupanda kwa vipandikizi kwani hutoa mizizi kwa shida sana (hii hata hivyo haitakiwi kuwa tatizo kwani kupanda kwa kutumia mbegu ni rahisi sana).

Kuhusiana na viini vya rutuba, mmea wa tumbaku haudai sana. Kwa kupata maua bora mengi, unaweza kuurutubisha mmea kwa mbolea kidogo na fosiforas kidogo zaidi.

««« Makala iliyopita: Kiwano – Cucumis metuliferus Makala inayofuata: Ukuzaji wa Uyoga chaza (Pleurotus ostreatus) »»»

Ijumaa 8.7.2011 15:38 | chapa | Mimea ya kigeni

Kuhusu KPR

KPR - Klabu ya Wakulima wa Bustani Slovakia
KPR - Klabu ya Wakulima wa Bustani ni shirika la kimataifa la wakulima wa bustani. Soma zaidi...
Shirikisha uzoefu wako kuhusu ukuzaji mimea. Andika makala kuhusu ukulima wa bustani, mimea, upandaji wa mimea nk. na uichapishe kwenye toleo la lugha yako la jarida letu la Botanix! Wasiliana nasi kwa taarifa zaidi.