Botanix – Jarida kuhusu mimea

Toleo la Kiswahili

Chai ya China – Lima chai yako mwenyewe!

foto

Chai ya China

Kabla ya kipindi cha baridi kumalizika, kila mkulima wa bustani anazingatia kipi ataota katika msimu ujao. Unaona hakuna changamoto tena kulima nyanya, pilipili mboga na tango? Unataka kitu kingine? Kitu kingine kisicho cha kawaida? Unafikiriaje wazo la kulima chai yako mwenyewe?!

foto

Mti wa chai (Camellia) una aina 50 za vichaka visivyokauka au miti midogo ambayo inajulikana sana kama mmea wa chai wa China (Camellia sinensis). Mti wa zamani asili yake ni Kusini na Kusini Mashariki mwa China na nchi jirani – India, Burma, Vietnam na Laos, ambako miti hii inalimwa kwa karne. Ingawa mti huu unalimwa katika vipindi vyote vya tropiki, wazalishaji muhimu sana watabaki kuwa China, India, Sri Lanka na Japan.

foto

Mbegu za chai

Kulima chai yako mwenyewe siyo kazi ngumu kamwe. Sehemu muhimu ya hatua ni kununua mbegu mpya, kwani mbegu za chai hupoteza uwezo wake haraka. Mbegu ni za duara. Kabla ya kupanda unatakiwa kuiloweka kwa muda wa siku 2 hadi 3. Baada ya hapo, lazima ipandwe kwenye udogo uliokauka vizuri na unaoingiza hewa. Kwenye hali joto ya nyuzijoto 20–25, mbegu huota ndani ya wiki 2–4. Kama ikipandwa kwenye sehemu yenye jua, mimea michanga hukua haraka na mimea ambayo ina umri wa miezi sita tu tayari inaweza kupogolewa. Shukrani kwa upogoaji sahihi, mtu anaweza kutengeneza taji zuri na kupata mali ghafi yako mwenyewe kwa kuzalisha mti wako mwenyewe.

Katika maeneo yenye joto kali au kidogo chai inaweza kupandwa kwenye bustani, lakini lazima iwekwe ndani ya nyumba au kwenye nyumba ya kuhifadhia mimea katika maeneo ambayo barafu hutokea. Joto kali na maji ya kutosha ni hali sahihi kwa mmea wa chai – hii ni hali ambapo hustawi katika nchi zake za asili.

Kama huishi kwenye maeneo yenye joto, hata kama chai ambayo unalima kwenye bustani yako mwenyewe au ubaraza inaweza isitosheleze ubora wa chai inayolimwa kwenye maeneo ya joto, utazawadiwa na furaha kubwa wakati mmea unapokuzawadia kwa kujali kwako na maua meupe mazuri makubwa.

Kama unaishi kwenye maeneo ambayo barafu hutokea, wakati wa baridi, lazima uweke mmea wa chai karibu na vizingiti vya madirisha. Kwasababu mmea wa chai haukauki na unaweza usipate jua la kutosha wakati wa baridi, unaweza kusinyaa na kupoteza majani kadhaa. Hata hivyo, kwa kuja kipindi cha uoto utaboreka haraka na utaweza kuchuma chai yako mwenyewe tena!

««« Makala iliyopita: Embe Kalimantan, Kasturi (Mangifera casturi) Makala inayofuata: Kiwano – Cucumis metuliferus »»»

Jumanne 5.7.2011 15:00 | chapa | Konifa

Kuhusu KPR

KPR - Klabu ya Wakulima wa Bustani Slovakia
KPR - Klabu ya Wakulima wa Bustani ni shirika la kimataifa la wakulima wa bustani. Soma zaidi...
Shirikisha uzoefu wako kuhusu ukuzaji mimea. Andika makala kuhusu ukulima wa bustani, mimea, upandaji wa mimea nk. na uichapishe kwenye toleo la lugha yako la jarida letu la Botanix! Wasiliana nasi kwa taarifa zaidi.